The House of Favourite Newspapers

DAKTARI: WEMA ANAHITAJI MASAJI

Wema Isaac Sepetu

DAKTARI ambaye ni mtaalam wa kuwa­fanyia watu masaji za mwili na viungo, Hap­piness Mtuya amesema kuwa staa wa filamu za Kibongo, Wema Isaac Sepetu anahitaji masaji ili mwili ukae vizuri baada ya kujipunguza.  Happiness ambaye anamiliki kliniki yake ya Happiness Masaji aliliambia Ijumaa kuwa, anatoa ofa ya mwaka ya kumfanyia masaji staa huyo bila malipo ili kuifanya mishipa yake ya damu ifanye kazi vizuri.

“Wema anahitaji masaji ili kuurudisha mwili wake sawa hivyo nampa ofa hiyo mwaka mzima aje tu kwenye kliniki yangu pale Lamata Hoteli, Ilala (Dar)” Daktari huyo aliongeza kuwa mastaa wengine aliowachagua kuwafanyia huduma hiyo ni Kajala Masanja na Aunt Ezekiel ambao wanaweza kuwasiliana naye kwa namba 0715 343161.

Stori: Imelda Mtema

Comments are closed.