The House of Favourite Newspapers

Dalali, Akilimali Washindana Kwa Mijengo Dar

Katibu wa Baraza la Wazee la Yanga, Yahya Akilimali.

UKIZUNGUMZIA wazee maarufu katika mchezo wa soka hapa nchini, bila shaka huwezi kuacha kuwataja aliyekuwa Mwenyekiti wa Klabu ya Simba, Hassan Dalali na Katibu wa Baraza la Wazee la Yanga, Yahya Akilimali.

Nyamba na Mzee Akilimali.

Hiyo ni kutokana na umaarufu mkubwa walionao katika soka la Tanzania lakini pia kuwa na wafuasi wengi ukilinganisha na wazee wengine wanaojihusisha na mchezo huo kwanjia yoyote ile hapa nchini.

Hata hivyo, licha ya umaarufu wao huo lakini maisha wanayoishi siyo ya kifahari ukilinganisha na ukubwa na majina yao katika tasnia ya soka hapa nchini.

Nyumba ya Mzee Mwambelo.

Wanaishi maisha ya chini na ya kawaida sana kama ambayo wanaishi Watanzania wengine wa kawaida kabisa ambao hawana umaarufu wowote.

Aliyekuwa Mwenyekiti wa Klabu ya Simba, Hassan Dalali.

Championi Jumatano limeweza kufanya uchunguzi wake umeibuka na kufahamu maisha wanayoishi wazee hao ambao ni maarufu kabisa katika soka la Tanzania ambao pia wana wafuasi wengi na hususan katika klabu za Simba na Yanga.

Mbali na hao, pia kuna wazee wengine wamefikiwa na Championi ambao ni aliyekuwa mmoja wa viongozi wa Baraza la Wadhamini wa Simba, Hamis Kilomoni pamoja na Juma Mwambelo ambaye ndiye anayedaiwa kuwa na hati ya Jengo la Yanga lililopo Mtaa wa Mafia, Kariakoo jijini Dar es Salaam.

Nyumba ya Mkwasa.

Mzee Dalali
Makazi ya Mzee Dalali yapo Magomeni Makanya jijini Dar, nyumba anayoishi ni ya kawaida ambayo ukiiangalia na ukalinganisha na ukubwa wa jina lake katika soka la Tanzania hususani Klabu ya Simba ambayo ameifanyia mambo makubwa wakati alipokuwa akiongoza, ni vitu viwili tofauti.

Wapo walioamini kuwa kutokana ukubwa wa jina lake pengine angekuwa na maisha mazuri na ya kifahari, lakini siyo hivyo.

Mzee Akilimali
Wengi wanamjua kwa mambo yake ambayo amekuwa akiyafanya kuhusiana na Yanga, kubwa zaidi ni jinsi alivyokuwa akipinga klabu hiyo kukodishwa na aliyekuwa mwenyekiti wa klabu hiyo, Yusuf Manji.

Nyumba ya Dalali.

Ilifikia wakati Mzee Akilimali alidai kuwa hata kama Manji ataondoka klabuni hapo yeye ana uwezo wa kuendesha klabu hiyo kwani ana uwezo mkubwa kifedha, lakini maisha anayoishi ni ya chini ukilinganisha na kile alichokuwa akikisema. Nyumba yake ipo Tandale kwa Mtogole jijini Dar es Salaam.

Mzee Kilomoni
Hivi karibuni wakati Simba inafanya mabadiliko ya mfumo wa uendeshaji wa klabu hiyo kutoka katika mfumo wake wa zamani wa wanachama na kuingia kwenye ununuaji hisa, Mzee Kilomoni alikuwa ni gumzo kubwa.

Nyumba ya Mzee Kilomoni.

Gumzo lake lilikuwa pale ambapo alipotofautiana kimtazamo wa Wanasimba wenzake na alikuwa akiungwa mkono na baadhi ya Wanasimba juu ya kile anachokisimamia. Mwisho wa siku akashindwa katika hoja yake hiyo. Simba hivi sasa imeingia kwenye mabadiliko.

Yeye mazingira anayoishi ni tofauti kidogo na wenzake. Nyumba yake ipo Kinondoni jijini Dar es Salaam ambayo ni ya kiwango cha juu tofauti na wazee waliopita hapo juu.

Mzee Mwambelo
Yeye anaishi Magomeni Makuti jijini Dar. Licha ya kudaiwa kuwa ndiye anayemiliki hati za Jengo la Yanga lililopo Mtaa Mafia, Kariakoo jijini Dar es Salaam tangu mwaka 1980 baada ya kuyumba kwa uongozi wa klabu hiyo, lakini maisha yake ni ya kawaida kabisa.
Nyumba anayoishi ni ya kawaida tofauti na wengi walivyokuwa wakifikiria kutokana na namna jina lake lilivyo.

Na Waandishi Wetu

Comments are closed.