The House of Favourite Newspapers

Dangote: Hatuna Mpango wa Kufunga Kiwanda Tanzania

0

Uongozi wa Kiwanda cha Saruji cha Dangote Tanzania kilichopo Mkoani Mtwara jana Febuari 16, 2021 kimekanusha taarifa za uvumi wa kukifunga kiwanda hicho zilizosambaa kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii.

 

 

Akizungumza na waandishi wa habari Mkurugenzi Mtendaji Abdullah Baba amesema Kiwanda cha Dangote kipo imara katika Uzalishaji na kinaendelea kutoa huduma huku ikifanya uzalishaji kufikia tani 5000 kwa siku tangu walipoanza kutumia nishati ya Gesi asilia.

 

 

Aidha, Abdullah Baba amesema kuna taarifa zisizo rasmi zinazosambaa mitandaoni dhidi ya kiwanda hicho za kutaka kukifunga hivi karibuni kuwa taarifa hizo sio za kweli ni uvumi tu.

 

 

Katika hatua nyingine Meneja Mahusiano ya jamii katika kiwanda hicho ndugu Siraji Nalikame amesema kuwa Dangote Tanzania imekuwa na ushirikiano mkubwa unaotolewa na Mamlaka za Serikali ya Mkoa, wilaya ya Mtwara pamoja na Wizara ya Viwanda na Biashara katika kutatua changamoto na kuongeza tija katika Uzalishaji.

Leave A Reply