Dankidanki Auawa Na Kukatwa Sehemu nyeti Kwa Kosa La Kumlawiti Mgonjwa – Video
Kijana mmoja aliyejulikana kwa jina moja la Wakudankidanki, mkazi wa Kinondoni Shamba, mwishoni mwa wiki iliyopita alifanya kitendo cha kinyama na kuumiza sana baada ya kumlawiti mama mmoja, Martha Sanga ambaye ni mgonjwa aliyepooza ambaye hawezi hata kujigeuza mwenyewe.
Wakizungumza na Global Tv, kwa nyakati tofauti walisema kuwa Kijana huyo aliingia kwenye chumba alicholala mgonjwa na kudhani kuwa kulikuwa hakuna mtu na kuanza kumlawiti huku akikazana kumchomoa mpira wa mkojo aliovaa, ambapo mgonjwa aliaanza kupiga kelele ndipo mpangaji mwingine alisikia ambaye naye mgonjwa amelala ndani.
“ Nilimkuta yuko juu ya mwili wa mgonjwa nikawa namvuta ananiambia nitakuchoma kisu, lakini nilijitahidi japo nilikuwa sina nguvu kwasababu naumwa,nilifanikiwa kumtoa alipotoka hapo akaanza kunipiga ngumi nikadondoka,nikapiga kelele watu wakaja na kuanza kumpiga ” alisema shuhuda huyo.
Jamani huyu mgonjwa ana wakati mgumu sana na maisha yake duni na bado hajapata matibabu sahihi tunaomba tumsaidie na mwenye nyumba amewapa siku tatu tu na hicho chumba kimoja wanalala wote,namba ya msaada ni 0693 964289 (HALIMA SANGA)