Dar Live Kuja na Usiku wa Piga Pikupige Idd Mosi

KATIKA kusherehekea Sikukuu ya Idd Mosi (Agosti 22, mwaka huu), Uwanja wa Taifa wa Burudani, Dar Live uliopo Mbagala-Zakhem jijini Dar umekuja na shoo bab’kubwa inayokwenda jina la Usiku wa Piga Nikupige ambapo Bendi za Muziki wa Taarab, Jahazi Modern pamoja na Zanzibar Stars zitachuana vilivyo.

Akizungumza na Mikito Nusunusu, Meneja na Mratibu wa Dar Live, Rajabu Mteta ‘KP Mjomba’ alisema kuwa, usiku huo shoo nzima inatarajia kuanza ‘mishale’ ya saa 12:00 jioni na kuendelea.

“Utakuwa ni usiku wa piga nikupige, wote tunaijua Jahazi Modern ilivyo kongwe na tishio lakini pia wote tunaijua Zanzibar Stars ilivyo kwa hiyo siku hiyo Zanzibar Stars wakiweka Utakiona Kimbembe na Twabonyeza Kibongobongo huku Jahazi Modern wanabandika Nia Safi Hairogwi na Kamwe Siumbuki, unakifiki itakuwaje? Njoo Dar Live.

“Lakini pia tutakuwa na Bendi ya Hurricane inayotikisa jijini Dar kwa kupiga live band ambapo usiku huo itapiga kopi ya nyimbo zote kali zinazotamba duniani,” alisema KP Mjomba.

Mbali na uwepo wa shoo hiyo, KP Mjomba aliongeza kuwa, siku hiyo kuanzia asubuhi kutakuwa na burudani kwa watoto ambapo Dar Live imewaandalia michezo mbalimbali kama vile Ngoma za Asili, Sarakasi, Kucheza na Nyoka, Moto huku kundi kabambe la Sarakasi na Mazingaombwe Wakali Dancers likigawa zawadi kibao.

STORI: MIKITO NUSUNUSU


Loading...

Toa comment