Usiku wa Uswazi: Hii Shughuli si ya Kitoto

UWANJA wa Taifa wa Burudani, Dar Live uliopo Mbagala-Zakhem jijini Dar kwa kushirikiana na Manywele Entertainment, unatarajiwa kuja na Usiku wa Uswazi na Nyonga za Motomoto kuanzia Alhamisi hii (Feb.1).

Mratibu wa usiku huo, Maimartha Jesse, aliiambia Risasi Vibes kuwa, shoo hiyo itakuwa kila Alhamisi ambapo wakali kibao watakuwepo akiwemo mkali wa Taarab, Khadija Kopa, wakali wa Singeli, Jack Simela pamoja na Msagasumu.

“Tutakuwa na makempu mbalimbali ambayo yatashindana kufunikana na niwaambie tu usiku huo utakuwa ukipambwa kwa nyonga motomoto kutoka kwa wenye shepu zao wakitoa Baikoko na Kibao Kata huku nao Super Maya wakifanya yao. Pia tutakuwa na zawadi kibao kutoka Manywele,” alisema Maimartha.

Naye Meneja wa Dar Live, Rajab Mteta ‘KP Mjomba’ aliongeza kuwa, shoo nzima itakwenda kwa mtonyo wa buku tano tu (5,000) getini.

“Lengo ni mashabiki wapate burudani na ndiyo maana tumeamua kushusha kiingilio kumuwezesha kila mmoja kuhudhuria. Nadhani kwa kiingilio cha 5,000 kila mmoja atafika na kufurahia,” alisema KP Mjomba.

 

Risasi Vibes


Loading...

Toa comment