The House of Favourite Newspapers

Darasa la 7 Waliozindua Mitambo ya Kufua Umeme Wamkosha JPM – Video

Rais wa Tanzania, John Magufulia amesema wakati akiwa Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi aliwahi kumuweka Meneja wa Wakala wa Ufundi na Umeme (Tamesa) Mkoa wa Kagera aliye na elimu ya darasa la saba.

Hayo ameyasema leo Alhamisi Juni 13, 2019 katika mkutano uliofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam ambapo alikutana na wabunifu wa kufua umeme kwa kutumia mitambo midogo Jairos Ngailo na John Mwafute ambao ni wakazi wa vijiji vya Msete na Lugenge mkoa wa Njombe katika.

Magufuli amesema sababu kubwa ya kumuweka darasa la saba ni kutokana na ukusanyaji wake mzuri wa kodi vizuri kuliko wenye shahada.

“Nielezee mipango yako vizuri ili nisije kumteua mmoja akawa Meneja Uzalishaji Tanzania na mwingine nisije kumteua akawa Meneja Usambazaji wa Tanesco,” amesema.

 

Awali, akizungumza katika mkutano huo, Mwafute amesema licha ya kuwa na elimu ya darasa la saba lakini aliweza kufanikiwa kutengeneza mtambo mdogo wa kufua umeme kwa ajili ya matumizi ya nyumbani.

“Kutokana na nia niliyokuwa nayo niliweza kusaidiwa na wahandisi wa Kijerumani ili kutimiza azma hii na hadi hivi sasa nilipofikia,” amesema Mwafute ambaye anazalisha umeme KV 28

MSIKIE MAGUFULI HAPA

Comments are closed.