The House of Favourite Newspapers

Darassa Aonywa Kujiunga WCB

WAKATI kukiwa na tetesi za mkali wa muziki,  Shariff Thabeet anayetamba na kibao cha Muziki kutaka kusainiwa katika lebo maarufu ya WCB, mtabiri maarufu nchini, Hassan Yahya Hussein amemuonya kuwa akithubutu kufanya hivyo, amekwisha.

Akizungumza na Risasi Vibes ofisini kwake Magomeni-Mwembechai, mtabiri huyo alisema nyota ya Darassa ni ya Mizani ambayo huwa ni mtu wa muziki, ambapo anatakiwa kusimama yeye kama yeye.

“Darassa akikubali kuwa chini ya mtu itakuwa ndiyo mwisho wake kimuziki maana nyota yake ni kali sana, haitakiwi kuongozwa na mtu maana mwenyewe anaweza kujiongoza, akizingatia hayo mwaka huu utakuwa ni wa mafanikio makubwa kwake  kwa  jumla,” alisema Hussein.

Save

Comments are closed.