The House of Favourite Newspapers

Darassa, Snura Kufanya Shoo Ya Kishindo Chato

0
Staa wa Bongo Fleva, Sharif Thabeet ‘Darassa’.

WAKALI wasioshikika kunako gemu la Muziki wa Bongo Fleva, Snura Mushi ‘Mamaa Majanga’ na Sharif Thabeet ‘Darassa’ Jumamosi hii (Agosti 5) wanatarajiwa kufanya  shoo ya kishindo katika uzinduzi wa hoteli ba’kubwa ya JS Motel iliyopo Chato mjini mkoani Geita.

Msikie Darassa

Akizungumza na Showbiz, Darassa anayebamba na Ngoma ya Hasara Roho alisema kuwa, siku hiyo ataonesha burudani ya kutosha kutoka kwa wateja na waalikwa wote watakaofika katika uzinduzi.

“Huwa sikosei linapotokea suala la mualiko kama hili la uzinduzi. Nashukuru kuwa miongoni mwa watakaozindua JS Motel ndani ya Chato Mjini kwa mara ya kwanza na ninachoahidi ni kufanya makamuzi ya live jukwaani nikipiga nyimbo zangu zote ikiwemo Too Much, Sikati Tamaa, Weka Ngoma pamoja na ngoma yetu hii ya taifa ya Muziki,” alisema Darassa.

Staa wa Bongo Fleva, Snura Mushi ‘Mamaa Majanga’ akifanya yake Dar Live.

Snura naye huyu hapa!

Kwa upande wa Snura ama Mamaa Majanga kama wengi wanavyomuita alisema, siku hiyo ya uzinduzi atafanya tukio ambalo si la nchi hii kutokana na alivyojiandaa.

“Mashabiki wote wanaifahamu shughuli yangu nikiwa katikati ya jukwaa. Tena hii imekuja mahala pake kwani nitawazindulia ngoma yangu mpya hukohuko kwenye uzinduzi wa JS Motel, asikwambie mtu yaani nitakinukisha mwanzo mwisho, kuanzia Chura, Najibadua, Shindu, Ushaharibu, Majanga na nyingine kibao.

Siyo kuwaimbia tu, siku hiyo nitawapa staili mpya ya kucheza nyimbo hizo ikiwemo na ya sasa ya Nionee Wivu niliowashirikisha Yamoto Band,” alisema Snura ambaye atakuwa na timu yake nzima ya madensa namba moja kwa kukata nyonga jijini Dar

Leave A Reply