Darleen: Hee! Ndoa yangu imevunjika!?

NILIJUA tu hawezi kudumu kwenye ndoa!” Ni maneno yaliyosambaa kwenye mitandao ya kijamii wikiendi iliyopita ikidaiwa kuwa, ndoa ya msanii wa Bongo Fleva, Mwanahawa Abdul ‘Queen Darleen’ imevunjika, lakini mwenyewe ameshangaa na kuhoji; “Hee! Ndoa yangu imevunjika!?”

Darleen ameiambia OVER ZE WEEKEND kuwa, habari hizo hazina ukweli wowote kwani ndiyo kwanza penzi lake na mumewe, Isihaka Mtoro limenoga.

STORI: HAPPYNESS MASUNGA

Toa comment