Darleen: Nilikuwa Chauroho Ile Mbaya
IMEFUNUKA! Ndivyo ambavyo unaweza kusema baada ya mwanamuziki kutoka Lebo ya Wasafi Classic Baby (WCB) Mwanahawa Abdul ‘Queen Darleen’ kufunguka kuwa, alipokuwa mdogo alikuwa chauroho kwani alipenda sana kukomba chakula akiwa anakula na watu wengi.
Akizungumza na Ijumaa Wikienda, Darleen alisema alifikia hatua ya kuonekana na tabia hiyo kwani kila alipokuwa anakula kwenye sahani au sinia na wenzake, alikuwa akikomba chakula na kujikusanyia upande wake.
“Nilikuwa na tabia mbaya sana, yaani tukiwa tunakula wengi kwenye sinia halafu nione kama wananizidi spidi, naanza kukomba chakula, najikusanyia upande wangu yaani nilikuwa mroho kupitiliza, ila mama yangu aliikomesha hiyo tabia kwa sababu ilikuwa ikitia aibu mbele za watu,” alifichua Darleen huku akicheka.
Stori: Shamuma Awadhi
Comments are closed.