Darleen Siyo Mke wa Kuachika

 

FIRST lady wa Wasafi Classic Baby (WCB), Mwanahawa Abdul ‘Queen Darleen’ ambaye juzikati alifunga pingu za maisha na mfanyabiashara Isihaka Mtoro, amesema baadhi ya watu wanadhani hataiweza ndoa, lakini anawaapia kuwa yeye si mke wa kuachika.

Darleen ameiambia Over Ze Weekend kuwa, siyo kila mwanamke wanayemuona, hawezi kuishikilia ndoa yake hadi anazeeka labda ni vile tu hawajapata nafasi ya kuwa na waume.

 

“Niwahakikishie tu kwamba hata kama nimeolewa mke wa pili, mimi siyo mke wa kuachika,” amesema Darleen aliyeolewa na Mtoro anayetajwa kuwa na ukwasi wa kubadilisha mboga.

STORI: IMELDA MTEMA

 

 

Toa comment