David Silinde Azidi Kuiteka Tunduma

Mgombea Ubunge kwa tiketi ya CCM Jimbo la Tunduma lililopo Mkoani Songwe, aDavid Silinde amezidi kuchanja mbuga katika kampeni zake baada ya jana Octoba 15, 2020 kufanya kampeni kata ya Mwaka Uwanjani iliyopo katika mji wa Tunduma.

Katika mkutano huo David Silinde akiwa ameambatana na Meneja wa kampeni zake, Aden Mwakyonde ambaye pia alikuwa mtia nia ya Ubunge Jimbo hilo, walielezea sababu za CCM kutakiwa kuchaguliwa Tunduma.

 

Kwa upande wake Mwakyonde alisema Jimbo la Tunduma limekuwa katika wakati mgumu kwa miaka mitano hivyo ni wakati sasa wa kumchagua David Silinde.

“Miaka mitano Jimbo hili lilikuwa katika upinzani na mmeona shida zilivyotukumba Tunduma ni mji mkubwa lakini haufanani na jina la Tunduma, Rais Magufuli katuletea miradi mikubwa Tunduma hivyo tumchague Davidi Silinde ili tupate miradi mingine mikubwa zaidi Tunduma,” alisema Aden Mwakyonde.

Kwa upande wake Davidi Silinde aliwataka wananchi wa Tunduma kumtuma Bungeni ili aweze kuwatumika na kushiriki katika vikao vya bajeti vya bunge hilo.

“Nitumeni Bungeni nikadai maendeleo ya Tunduma,nikamsaidie Rais Magufuli kazi mimi ni tofauti na aliekuwa Mbunge wa Jimbo hilo yeye vikao vya bajeti bungeni alitoka nje hivyo ni vingi vimetupita Wana Tunduma” alisema Silinde.

 

Katika Mkutano huo wananchi wa Tunduma walijitokeza kwa mamia kusikiliza Mkutano wa Kampeni na walimgomea Silinde kupanda gari hivyo walimsindikiza mpaka ofisi za chama kwa kucheza njia nzima mwendo wa kilometa 2.

Na Rahim Nzunda

Toa comment