David Silva Ajiandaa Kutimkia Valencia
KIUNGO wa Manchester City, David Silva ameanza mazungumzo na klabu ya Valencia ili aweze kujiunga nayo mwishoni mwa msimu huu.Silva anamaliza mkataba wake na Manchester City mwishoni mwa msimu huu na ameshasema kuwa hataendelea kuitumikia timu hiyo tena.
Staa huyo ni kati ya wachezaji waliopata mafanikio makubwa kwenye kikosi cha City akiwa amekaa hapo kwa zaidi ya miaka kumi.Silva mwenye miaka 34, anataka kwenda kumalizia soka lake kwenye kikosi cha Valencia ambacho alitokea na kujiunga na City.
Mazungumzo yanaelezwa kuwa yamekuwa yakifanya na yapo kwenye muelekeo mzuri kwa staa huyo raia wa Hispania


