DAVIDO AWEKA REKODI HII

MKALI wa muziki Ni ­geria, Davi­do amewe­ka rekodi nchini humo kwa kuwa mwanamuziki wa kwanza kufikisha wafuasi milioni 9 katika ukurasa wake wa Instagram.  Kwa sasa Davido ndiye staa anayekimbiza kwa wafuasi hao akifuatiwa na Wizkid mwenye wafuasi milioni 7 kisha Tiwa Sav­age mwenye milioni 6.5.

Ikumbukwe kuwa, Davido aliweka rekodi ya mwanamuz­iki wa kwanza nchini humo kufikisha ‘likes’ laki tano kwa posti moja. Ameweka rekodi nyingine ya kufikisha ‘likes’ milioni moja kwa posti moja ambapo mara ya mwisho aliposti kipande cha video aliyokuwa anaandaa muziki akishirikiana na msanii mwenzake, Zlatan Ibile.

 

JIUNGE NA FAMILIA YA GLOBAL TV UPANDE MTANDAO WA MAFANIKIO

Bofya hapa kujiunga na familia ya Global TV Club ==> Global TV Family Club


Loading...

Toa comment