The House of Favourite Newspapers

#GlobalCelebrityUpdates: Davido Azianika Sababu Za Kutemana Na Lebo Ya SONY

Baada ya kujitoa kwenye label ya muziki ya Sony, Davido amejitokeza kuzungumza sababu zilizomsukuma kufanya maamuzi hayo.

Kwenye pitapita yangu Instagram nimekutana na post ya Davido kwenye page yake ya Instagram ikielezea sababu zilizomfanya achukue maamuzi ya kujikata na lebo kubwa ya muziki kutoka Marekani Sony.

Kwa mujibu wa staa huyo wa Nigeria, Sony walisema kuwa aina ya muziki anaouimba Davido hautoweza kumpatia soko analolitaka Marekani hivyo kumtaka abadilishe aina muziki anaoufanya kama anataka kupenya kwenye soko la kimataifa. 

Kupitia Instagram page yake, Davido alishare video ya msanii wa Marekani Omarion akiimba wimbo wake mpya ‘IF’ na kuandika caption ifuatayo:

Bro Omarion amezikubali vibes za ‘IF’!… Mwaka jana mzima, walijaribu kuubadilisha muziki wangu… wakidai mimi kubaki na sound yangu ya Kiafrika isingeweza kunipa manufaa yoyote nje ya Africa! Mwaka huu niliwaomba na kuwalazimisha waniruhusu nifanye muziki ninaoujua kuufanya sasa ona kinachotokea!! MUZIKI HAUNA LUGHA!! NA KWA MARA NYINGINE TENA NINA HIT KUBWA KULIKO ZOTE AFRICA! THANKS TO JAH!! ” 

‘IF’ kwa sasa inafanya vizuri sana kwenye chati za muziki Nigeria na sehemu nyingine za Africa, na pengine Omarion kujipost akiuimba wimbo huo ni dalili kubwa za single hiyo kuwa hit nyingine ya Africa kutawala kwenye soko la muziki la kimataifa.

Sony bado hawajasema chochote kuhusu post ya Davido na haijajulikana kama watachukua hatua zozote dhidi ya msanii huyo.

Imeandikwa Na: Sandra Brown.

Subscribe kwenye YouTube Chanel yetu ya Global TV Online ili zote kali zinazotufikia iwe ni siasa, michezo, comedy, burudani, stori za mastaamuziki na nyingine zikufikie kwa wakati.

Comments are closed.