The House of Favourite Newspapers

Davido, Burna Boy Wachapana Makonde Night Club – Video

0

MASTAA wawili wakubwa barani Afrika ambao wote ni raia wa Nigeria, Damini Ebunoluwa Ogulu ‘Burna Boy’ na mwenzake David Adedeji Adeleke ‘Davido’,  wameripotiwa kupigana huko nchini Ghana wakati wakiwa kwenye Night Club usiku wa kuamkia leo Jumatatu, Desemba 28, 2020.

 

Manguli hawa wa muziki wamekuwa na uhasama wa kurushiana maneno kwa muda mrefu kupitia mitandao ya kijamii, lakini jana mambo yalikwenda tofauti mpaka wakaamua kuvaana live.

 

 

Clip moja ya video kwenye mtandao wa Twitter imeonekana kuunga mkono ripoti hizo ambapo ilimnasa mtu mmoja mwenye hasira aliyeonekana kama Davido akimsukuma mtu mwingine ambaye alionekana kama Burna Boy.  Hata hivyo, sababu ya mapigano hayo haijaelezwa hadi sasa.

 

 

View this post on Instagram

 

A post shared by Global Publishers (@globalpublishers)

Leave A Reply