The House of Favourite Newspapers

Davina Afungukia Kuidai CCM

Halima Yahaya ‘Davina’

Na BONIPHACE NGUMIJE| GAZETI LA UWAZI| SHOWBIZ 

MWANADADA anayefanya vyema kwenye tasnia ya filamu  nchini, Halima Yahaya ‘Davina’ hivi karibuni amefunguka kuwa kwa upande wake hakidai hata senti tano Chama Cha Mapinduzi (CCM), maana alipata alichostahili wakati wa kampeni.

Davina

Akichonga na Showbiz , Davina aliyekuwa miongoni mwa wasanii waliounda Kundi la Mama Ongea na Mwanao wakati wa Kampeni ya Uchaguzi Mkuu 2015, alisema kuwa sinema inayoendelea kati ya Steve Nyerere na Wema Sepetu pamoja na madai ya wasanii waliounda kundi hilo kuidai CCM hahusiki nayo na kila kinachoendelea yeye anakitazama kama walivyo watazamaji wengine.

“Kiukweli mimi siidai CCM chochote maana nilipata ninachostahili, kama kuna wasanii wengine wanaidai mimi sijui na hata kuhusu wasanii kumjibu Steve Nyerere kwa alichokisema kuwa hakuna msanii anayeidai CCM mimi nasikia tu kutoka kwa watu maana sihusiki kabisa,” alimaliza Davina

 

Hapa tumekuanikia kurasa za mbele na za nyuma za magazeti yote ya Tanzania leo, Februari 27, 2017. Ni yale ya Hardnews, Udaku na Michezo.

Kwa stori zote kali, Tu-follow

Facebook @Globalpublishers

Twitter @GlobalHabari

Instagram @GlobalPublishers

YouTube @GlobalTVTZ

Shinda Nyumba Awamu ya Pili Yatikisa Jiji la Dar es Salaam

Comments are closed.