Davina Afungukia Kuidai CCM
Na BONIPHACE NGUMIJE| GAZETI LA UWAZI| SHOWBIZ
MWANADADA anayefanya vyema kwenye tasnia ya filamu nchini, Halima Yahaya ‘Davina’ hivi karibuni amefunguka kuwa kwa upande wake hakidai hata senti tano Chama Cha Mapinduzi (CCM), maana alipata alichostahili wakati wa kampeni.
Akichonga na Showbiz , Davina aliyekuwa miongoni mwa wasanii waliounda Kundi la Mama Ongea na Mwanao wakati wa Kampeni ya Uchaguzi Mkuu 2015, alisema kuwa sinema inayoendelea kati ya Steve Nyerere na Wema Sepetu pamoja na madai ya wasanii waliounda kundi hilo kuidai CCM hahusiki nayo na kila kinachoendelea yeye anakitazama kama walivyo watazamaji wengine.
“Kiukweli mimi siidai CCM chochote maana nilipata ninachostahili, kama kuna wasanii wengine wanaidai mimi sijui na hata kuhusu wasanii kumjibu Steve Nyerere kwa alichokisema kuwa hakuna msanii anayeidai CCM mimi nasikia tu kutoka kwa watu maana sihusiki kabisa,” alimaliza Davina
Hapa tumekuanikia kurasa za mbele na za nyuma za magazeti yote ya Tanzania leo, Februari 27, 2017. Ni yale ya Hardnews, Udaku na Michezo.
Kwa stori zote kali, Tu-follow
Facebook @Globalpublishers
Twitter @GlobalHabari
Instagram @GlobalPublishers
YouTube @GlobalTVTZ
Comments are closed.