Davina ataja sababu kuanika upaja!

Gladness Mallya

MWIGIZAJI ambaye inaaminika kwa muda mrefu hajawahi kuvaa nguo yenye mpasuo kiasi cha mapaja yake kuonekana, Halima Yahya ‘Davina’, amefunguka kuwa kwa mara ya kwanza Jumapili iliyopita alilazimika kuvaa nguo iliyoonesha sehemu ya paja lake kutokana na mazingira ya pati ya mwigizaji mwenzake, Wema Sepetu ‘Madam’.

Akielezea vazi hilo alilolitinga katika sherehe ya kuzaliwa ya Madam, Davina alisema kwa mazingira ya pati hiyo yenye hadhi ya aina yake, alilazimika kuvaa nguo hiyo ili kuendana na mazingira lakini si kwamba amebadilika tabia yake.

“Jamani pale nilivaa tu kulingana na mazingira na hata hivyo haijaanika mapaja kihivyo, si kwamba ndiyo nimebadilika kitabia, kamwe siwezi kubadilika,” alisema Davina.


Loading...

Toa comment