The House of Favourite Newspapers

Davina: Nimemisi kupika futari ya familia

0

davinaNa Hamida Hassan, Ijumaa

Dar es Salaam: Staa wa sinema za Kibongo, Halima Yahya ‘Davina’ amefunguka kuwa amemisi kupika futari mwaka huu kwa kuwa muda mwingi yuko lokesheni na kubwa zaidi ni kwa sababu hana mume wa kumpikia futari kama miaka iliyopita.

Akizungumza na Ijumaa, Davina alisema kuwa mwaka huu amekuwa akila futari nyumbani kwa watu mbalimbali na kuzifaidi tofauti na miaka ya nyuma ambapo alikuwa bize kumpikia mumewe ambaye wamemwagana.

Paparazi wetu alimuuliza Davina kama ana mpango wa kuolewa tena hivi karibuni ambapo alisema kwa sasa halitegemei hilo kwani anachoangalia ni kazi kwanza.

“Kiukweli nimemisi kupika futari lakini kwa sasa mimi napiga kazi na kuwalea watoto wangu,” alisema Davina.

Leave A Reply