DAVINA: ACHEKELEA UBALOZI WA WATOTO WA MTAANI!

STAA wa Filamu za Kibongo, Halima Yahaya ‘Davina’ hivi karibuni ameteuliwa kuwa balozi wa watoto wa mtaani na Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Patrobas Katambi ambapo mwenyewe ameeleza kufurahishwa kwake na uteuzi huo.

 

Akizungumza na Ijumaa Wikienda, Davina alisema amefurahi kupewa nafasi hiyo kwa sababu kupitia ukatibu wake kwenye Chama cha Wanawake wa Tasnia ya Filamu anaamini watawasaidia watoto hao kufikia ndoto zao.

 

“Unajua baada ya kuteuliwa kuwa balozi nimeona ni jambo la furaha kwani sisi wanawake kupitia chama chetu tumekuwa tukifanya shughuli za watoto na akina mama, kwa maana hiyo tutaandaa tamasha kubwa kwa ajili ya kujua vipaji vyao kisha tuwasaidie kufikia ndoto zao,” alisema Davina.

 

Aidha Davina alisema watakapoandaa tamasha hilo watawapata watoto wenye vipaji vya uigizaji, wacheza mpira, wanamuziki hivyo watawasaidia kwa namna moja au nyingine kuwaweka karibu kwenye fani zote hizo hili wafanikiwe na pengine watakuwa wamewasaidia kutoka mtaani.

Loading...

Toa comment