The House of Favourite Newspapers

Dawasco kuzima mtambo wa maji wa ruvu chini kwa siku mbili

0

AqXREzz1S0UGZvNzQMPt-TFoMMHMLHoCGNRKr3z_DmTo

Afisa Uhusiano wa Shirika la Maji Safi na Majitaka Dar es salaam (DAWASCO), Everlasting Lyaro, akizungumza na wanahabari (hawapo pichani) wakati akitoa taarifa ya kuzimwa kwa Mtambo wa kuzalisha Maji wa Ruvu Chini kwa wastani wa Saa 48 kwa siku za Jumamosi 23/01/2016 na Jumapili 24/01/2016

Mtambo wa Ruvu Chini utazimwa ili kuruhusu Mkandarasi Kuunganisha bomba Jipya na Bomba la zamani katika tanki la Maji Wazo- Tegeta. Zoezi hili linaashiria kuanza kukamilika kwa upanuzi wa Mtambo wa Maji wa Ruvu Chini ambapo Shirika linakusudia kuzalisha Maji mapya toka kiwango cha sasa cha cubic za ujazo 182,000 hadi cubic 270,000 kwa siku kuanzia mwezi Februari 2016 na Kuondoa kabisa tatizo la Maji kwa maeneo yanayohudumiwa na Mtambo wa Ruvu Chini.
Kuzimwa Kwa mtambo wa Ruvu Chini kutapelekea maeneo yafuatayo katika Jiji kukosa Maji:. MJI WA BAGAMOYO VIJIJI VYA ZINGA, KEREGE NA MAPINGA, BUNJU, BOKO, TEGETA, KUNDUCHI, SALASALA, JANGWANI, MBEZI BEACH NA KAWE.Maeneo Mengine ni : MLALAKUWA, MWENGE, MIKOCHENI, MSASANI, SINZA, KIJITONYAMA, KINONDONI, OYSTERBAY, MAGOMENI, UPANGA, KARIAKOO, CITY CENTRE, ILALA, UBUNGO MAZIWA, KIGOGO, MBURAHATI, HOSPITALI YA RUFAA MUHIMBILI, BUGURUNI, CHANGOMBE NA KEKO.
WANANCHI MNASHAURIWA KUHIFADHI MAJI NA KUYATUMIA KWA MATUMIZI YA LAZIMA.
Wasiliana nasi kupitia kituo cha huduma kwa wateja 022-2194800 au 0800110064 (BURE)DAWASCO INAWAOMBA RADHI WANANCHI KWA USUMBUFU UTAKAOJITOKEZA.
IMETOLEWA NA OFISI YA UHUSIANODAWASCO-MAKAO MAKUU

Leave A Reply