The House of Favourite Newspapers

Dayna Akumbwa na Gonjwa la Kuweweseka

0
Staa wa Bongo Fleva, Mwanaisha Saidi ‘Dayna Nyange’.

Na Boniphace Ngumije | Uwazi | Habari
STAA wa Bongo Fleva, Mwanaisha Saidi ‘Dayna Nyange’ amefunguka kuwa siku za hivi karibuni amekumbwa na gonjwa la kuweweseka linalomkosesha raha.
Akipiga stori na Uwazi Showbiz, Dayna alieleza kuwa kuweweseka huko kunatokana na msongo wa mawazo alionao kwani anawaza kazi mpya atakayoitoa baada ya Wimbo wa Komelo kuendelea kufanya vizuri kwani muziki kwa sasa una ushindani mkubwa mno.

“Kiukweli ninavyowaza kuhusu ujio mpya mpaka najikuta naweweseka usiku wakati nikiwa nimelala, nikishtuka natuliza mawazo na kujipa moyo kuwa Mungu atanisaidia nitaandaa kazi nzuri ambayo itafika mbali zaidi ya hii niliyotoa sasa,” alisema Dayna.

Leave A Reply