The House of Favourite Newspapers

Dayna Awalilia Watanzania Tuzo za Bae

dayna-1

Na Risasi Januari 18

MWANADADA anayefanya poa kwenye Muziki wa Bongo Fleva, Mwanaisha Said ‘Dayna Nyange’ amewalilia Watanzania kumsapoti kwa kumpigia kura katika Tuzo za Bae zitakazofanyika hivi karibuni nchini Nigeria, ambapo amewekwa kushindania kipengele cha Best African Act.

 dayna-3

Dayna anayebamba na Ngoma ya Komela alisema kuwa, hana kimbilio lingine la kwenda kuomba kura zaidi ya mashabiki wa muziki nchini, bila kujalisha wanapenda kazi zake au la, huku akiwataka kutanguliza uzalendo mbele.

“Ninatumaini kazi zangu zinakubalika ndiyo maana nimeweza kuchaguliwa kushindania tuzo hizo za Bae, naomba sana Watanzania wanipe sapoti niweze kuibuka mshindi ambapo utakuwa ni mwendelezo wa mimi kufanya vizuri zaidi nje ya nchi,” alimaliza Dayna.

Comments are closed.