D’Banj: Olamide si mwizi

imageHATIMAYE, mwimbaji maarufu wa Nigeria, D’Banj, amejibu tuhuma za prodyuza wa muziki, Dee Vee, anayemiliki kampuni ya DB Records kwamba rapa Olamide aliiba mistari kadhaa ya wimbo wake (DeeVee).

Itakumbukwa na wafuatiliaji wa muziki kwamba wiki kadhaa zilizopita, DeeVee alisema Olamide aliiba mstari kutoka katika wimbo wa D’Banj uitwao ‘Shake It’ ambao bado haujatoka.

Hata hivyo, D’Banj amesema hawezi kukiita kitendo hicho kuwa ni wizi bali ni changamoto njema. Alisema kwamba nyumba yake iko wazi kwa msanii yeyote kwenda na kusikiliza nyimbo zake ambazo bado hazijatoka.

Alisema: “Sikuufahamu ujumbe wa DeeVee, lakini ukweli ni ukweli. Nyumba yangu iko wazi; nina nyimbo ambazo hamjazisikia. Nina nyimb
o ambazo nitazitoa.

Hata hivyo, wakati wowote mtu anakaribishwa kuja katika studio zangu na kusikiliza nyimbo zetu; si Olamide tu bali watu wote. Kwangu kitendo hiki si wizi, bali changamoto nzuri.”

Maneno yanayodaiwa kuigizwa kutoka wimbo husika ni yale ya “Shake it, don’t break it, it took your mama nine months to make it.”

Loading...

Toa comment