Miriam Odemba akifanya mazoezi.
Washiriki mbalimbali wakiwa kwenye mazoezi.
Hapi na Odemba wakiwa kwenye mazoezi ya viungo.
DC Hapi akizungumza jambo baada ya kumalizika kwa mazoezi hayo katika Viwanja vya Posta Kijitonyama.
Baadhi ya washiriki wakiwa kwenye mazoezi kwenye Viwanja vya Posta, Kijitonyama.
Wakivuka Barabara ya Ali Hassan Mwinyi
Baadhi ya wanafunzi wa shule za msingi walioshiriki mazoezi hayo.
Baadhi ya wanafunzi wakifurahi na walimu wao.
MKUU wa Wilaya ya Kinondoni, Ali Hapi leo Machi 11, 2017 na mwanamitindo mahiri aliyewahi kuwa Miss Tanzania, Miriam Odemba wameshiriki mazoezi ya viungo na kukimbia (jogging), umbali wa kilomita 7 ambayo yalimalizikia kwenye Viwanja vya Posta, Kijitonyama jijini Dar es Salaam.
Mazoezi hayo ni mwendelezo wa kampeni ya kitaifa iliyoanzishwa na Makamu wa Rais, Samia Suluhu aliyowaagiza viongozi wa mikoa na wilaya zote kuweka utaratibu wa kufanya mazoezi angalau mara moja kwa mwezi kama kampeni ya kitaifa ya kudhibiti magonjwa yasiyoambukiza.
Akizungumza baada ya kumalizika kwa mazoezi hayo, Hapi alisema anawaomba wananchi wa wilaya yake wa kila rika kujitokeza kila mwisho wa mwezi kufanya mazoezi ya pamoja ili kuimarisha afya na kujenga mwili.
“Nawaasa wananchi mfanye mazoezi na muanzishe vikundi vya mazoezi na serikali itatimiza wajibu wake wa kuweka mazingira mazuri ya kufanyia mazoezi ikiwa ni pamoja na kutafuta wadau mbalimbali wa kufanikisha kupata wadau angalau wa kutuletea maji,” alisema Hapi.
Pia ameagiza walimu wa shule za msingi katika wilaya yake kuhamasisha wanafunzi kufanya mazoezi ya asubuhi kwa kukimbia mchakamchaka kwani yatawasaidia kuimarisha afya za wanafunzi na kukabiliana na magonjwa mbalimbali.
Na Denis Mtima/GPL
Comments are closed.