The House of Favourite Newspapers

DC ILALA AZINDUA UTARATIBU KUWATAMBUA MACHINGA KARIAKOO

Baadhi ya Wamachinga walioshiriki hafla hiyo.
Mkuu wa Wilya ya Ilala, Sophia Mjema, akizungumza na Wamachinga eneo la Kariakoo leo.

 

MKUU  wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema, leo amezindua utaratibu maalumu wa kuwatambua wafanyabiashara wadogowadogo maarufu kama Wamachinga  kwa kuwapatia vitambulisho vya taifa ili watambulike katika mabenki wakati wa kuomba mikopo kwa ajili ya kupanua wigo wa biashara zao.

 

Akizungumza katika uzinduzi huo  katika soko la Kariakoo, Dar es Salaam, Mjema amesema  serikali ya awamu ya tano inataka kuona   wafanyabiashara hao wanakua kiuchumi na hivyo  na hivyo kuwapa  uwezo wa kukopa katika mabenki kutokana na vitambulisho hivyo.

 

Naye mfanyabiashara katika soko la Kariakoo, John Mushi, ameipongeza hatua hiyo ya serikali kwani itasaidia kupunguza migogoro kati yao na mgambo wa jiji.

 

Comments are closed.