The House of Favourite Newspapers

DC Kiswaga Azindua Msimu Mpya Wa Kilimo Huku Mvua Ikinyesha

 

Mkuu wa Wilaya ya Bariadi Mkoani Simiyu Festo Kiswaga akigawa Mbegu bure kwa wananchi wa kata ya Nkololo, wakati wa sherehe za uzinduzi wa Msimu wa kilimo wilayani humo 2016/17.

…Akizungumza na wananchi hao.

Wananchi wa kata ya Nkololo wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Festo Kiswaga. (hayupo pichani).

 

Mkuu wa Wilaya ya Bariadi Mkoani Simiyu Festo Kiswaga (Kulia) akikata utepe kuashiria kuzinduliwa kwa msimu wa kilimo wilayani humo 2016/17, (kulia) ni Makamu Mwenyekiti wa Halmshauri ya Wilaya hiyo Duka Mashauri Mapya.

Mkuu wa Wilaya ya Bariadi Mkoani Simiyu Festo Kiswaga akigawa Mbegu kwa Mwenyekiti wa halmashauri ya Mji wa Bariadi Robert Rweyo (katikati) pamoja na Makamu Mwenyekiti wa halmashauri ya Wilaya Duka Mashauri Mapya.

Mkuu wa Wilaya ya Bariadi Mkoani Simiyu Festo Kiswaga akigawa Mbegu kwa Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) wilayani humo, wakati wa zoezi la uzinduzi wa msimu wa kilimo wilayani humo 2016/17.

Mkuu wa Wilaya ya Bariadi Mkoani Simiyu Festo Kiswaga akigawa Mbegu bure kwa wananchi wa kata ya Nkololo, wakati wa sherehe za uzinduzi wa Msimu wa kilimo wilayani humo 2016/17.

Mkuu wa Wilaya ya Bariadi Mkoani Simiyu Festo Kiswaga akigawa Mbegu bure kwa wananchi wa kata ya Nkololo, wakati wa sherehe za uzinduzi wa Msimu wa kilimo wilayani humo 2016/17.

Mkuu wa wilaya ya Bariadi Mkoani Simiyu Festo Kiswaga jana alilazimika kunyeshewa mvua akiwahamasisha wananchi wa wilaya hiyo kulima mazao kwa kitaalamu ikiwa pamoja na kugawa mbegu bure kwa baadhi ya wananchi pamoja na viongozi.

Hali hiyo ilitokea katika kata na kijiji cha Nkololo wakati Mkuu huyo wa wilaya alipokuwa akizindua msimu wa kilimo wilayani humo 2016/17, ambapo sherehe hizo zilihudhuliwa na viongozi wa halmashauri, madiwani pamoja na watendaji wote wakiwemo wananchi.

Kiswaga alisema kuwa ofisi yake imejipanga kuhakikisha wananchi wanalima na kupata mazao kwa kiwango kikubwa ili kuweza kuondokana na janga la Njaa ikiwa pamoja na kuachana na utamaduni wa kuomba chakula serikalini.

Alisema katika kuhakikisha suala hilo linafanikiwa aliagiza kila kaya kuhakikisha inalima hekari nne za mazao mbalimbai, huku kila hekari moja zao moja, ambapo aliyataja mazao yatakayopewa kipaumbele kuwa ni Mahindi, Pamba, Mbaazi pamoja na Choroko.

Alisema kila kaya itatakiwa kulima mazao hayo katika msimu huu na misimu mingine mbeleni, kama hatua ya kuazia katika mpango ambao alisema ameuanzisha Ushirikishwaji wa wananchi katika kilimo kuondoa umaskini na Njaa.

Alisema katika mpango huo uhakika umeonekana kuwa wananchi wa wilaya hiyo hawataomba chakula cha msaada kutoka serikalini, ikiwa pamoja na kukuza uchumi wao na jamii kwa ujumla kwa mazo ya biashara ambayo ni Mbaazi pamoja, Choroko pamoja na Pamba.

Aidha alisema kulima mazao hayo manne itakuwa lazima, ambapo aliwataka wananchi kutoa taarifa kwa haraka ofisini kwake au kwa viongozi wengine kwa wafanyabiashara au makampuni yatakayobainika kuuza na kusambaza mbegu na madawa feki.

” ninategemea wananchi wote mtaunga mkono mpango wangu huu ambao tunaanza na mazao ya aina nne, niwatake toeni taarifa kwa watu watakaowapatia mbegu na madawa feki, watalam wa halmashauri lazima kusimamia mpango kwa wananchi ili kuweza kuzalisha kwa kiwango kikubwa msimu huu” Alisema Kiswaga.

Awali akiongea Makamu Mwenyekiti wa halmashauri ya Wilaya Bariadi Duka Mashauri Mapya, alisema kuwa wananchi wa wilaya hiyo hasa wanaopakana na hifadhi ya Taifa Serengeti wamekuwa wakipata kero kubwa kutoka kwa wanyama hasa tembo kwa kuaribu mazao yao.

Alimuomba Mkuu huyo wa wilaya katika kutekeleza mpango huo suala la wanyama hao lazima kuangaliwa kwa kiwango kikubwa ikiwa pamoja na kupambana na watu wanaosambaza mbegu na madawa feki.

 

Comments are closed.