DC Magoti Alivyotatua Kero Za Wananchi Papo Hapo, Awapa Maagizo Watumishi Wa Umma – Video

Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Petro Magoti amepigilia msumari kauli yake aliyoitoa hivi karibuni ya kupiga marufuku watoto wadogo wa kike kuchezwa unyago wilayani humo na kusisitiza kwamba yupo ‘serious’.
Magoti ameyasema hayo leo kwenye mkutano wake wa kusikiliza na kutatua kero za wananchi wilayani humo na kueleza kwamba yeyote ambaye atatoa taarifa za kufichua wazazi wanaowacheza unyago mabinti zao, atampa zawadi ya shilingi 50,000.