The House of Favourite Newspapers

DC Magoti Atoa Tamko Pikipiki Haziruhusiwi Kubeba Mkaa – Video

0

Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Petro Magoti amepiga marufuku pikipiki (bodaboda) kutumika kusafirishia mkaa na kueleza kuwa sheria haziruhusu usafiri huo kutumika kubebea mkaa.

Magoti ameongeza kuwa, pia ni marufuku kwa magari yanayosafirisha mkaa, kutembea barabarani nyakati za usiku kwani sheria inaeleza kuwa mwisho ni saa 12 jioni.

Magoti amesema anasimamia sheria kwa sababu kumekuwa na wimbi kubwa la uvunaji wa misitu kiholela katika Wilaya ya Kisarawe, jambo ambalo linachangia ukosefu wa mvua za kutosha.

Leave A Reply