DC Mwanziva na Mashekhe Ludewa Wawafikia Kinamama Hospitalini
Mashehe wilayani Ludewa mkoani Njombe wamewaasa waumini wote wa kiislam hapa nchini kukumbuka kutoa zaka katika kipindi hiki cha ramadhani kwakuwa kipindi hiki kinahusiana na matendo ya huruma, pamoja na kujifunza mambo ikiwemo kutoa zaka kwa watu wa makundi mbalimbali.
Hayo ameyasema Shekhe wa wilaya hiyo Haruna Rahim mbele ya mkuu wa wilaya hiyo Victoria Mwanziva baada ya kuwasili katika hospitali ya wilaya ya Ludewa na kutembelea wodi ya wazazi na kutoa vitu mbalimbali kwa matumizi ya wazazi na watoto.
Aidha kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Ludewa Victoria Mwanziva amesema ameona ni vyema kujumuika na viongozi hao wa dini ikiwa ni njia mojawapo ya kufanya matendo ya huruma na kujenga imani ya kidini na wakaona ni vyema kuonyesha upendo wao kwa kuwatembelea wakinamama hao wajawazito na wanaosubiri kujifungua.
“Nimewaletea salamu kutoka kwa Rais wetu wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan rais ambaye anaupendo kwa akina mama na watoto pia hivyo mimi pamoja na mashekhe hawa katika kipindi hiki cha ramadhani tumekuja kuwapa salamu za upendo kutoka kwa rais wetu Dkt. Samia”
Aidha katika zoezi hilo limehusisha madaktari , wauguzi na baadhi ya watumishi kutoka ofisi ya wilaya hiyo.