Sabaya Awatia Ndani Wahasibu ‘Waliopiga’ Ada za Wanachuo – Video

SAKATA la wanachuo wa Chuo cha Ualimu Moshi limechukua taswira mpya baada ya Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya, kukutana na wadau wote waliotajwa kuhusika katika upotevu wa fedha za ada za wanafunzi walizolipa lakini hazionekani katika akaunti ya chuo hicho.

 

Hatua hiyo ni pamoja na kuwatia ndani wahasibu waliohusika katika mchakato ambao pesa hizo zilipitia.

 

Wanachuo hao zaidi ya 400 waliandamana juzi (Jumatatu) na kuziba barabara kushinikiza kulipwa fedha zao zaidi ya shilingi milioni 72 zilizolipwa kwa ajili ya ada kupitia wakala wanaojulikana kwa jina la ELCT-ND SACCOS Tawi la Moshi huku fedha zikiwa hazionekani kwenye akaunti ya chuo.

 

Baada ya kuwasikiliza wanafunzi hao, uongozi wa chuo,uongozi wa benki ya CRDB BANK,na kuwahoji wahasibu wa pande zote (chuo hicho na ELCT-ND SACCOS) Sabaya amewapa nafasi wahusika wote kukutana na kupitia kumbukumbu za nakala zote ili kujiridhisha kiasi kamili cha fedha zilizopotea ili Alhamisi wiki hii, pafikiwe mwafaka wa fedha za wanafunzi hao kurudishwa.

 


Loading...

Toa comment