testiingg
The House of Favourite Newspapers

De Bruyne Ashangazwa na Tuzo ya Mchezaji Bora wa Mechi Dhidi ya Canada

0
Nyota wa Ubelgiji Kevn De Bruyne

NYOTA wa Timu ya Taifa ya Ubelgiji na klabu ya Manchester City ya nchini Uingereza Kevin De Bruyne ameshangaa kukabidhiwa tuzo ya mchezaji bora wa mchezo kati ya timu yake ya Ubelgiji dhidi ya Canada kutokana na kuamini kuwa hakustahili kwa sababu hakucheza vizuri.

 

“Sidhani kama nilicheza vizuri, sielewi ni kwanini nimepata hii tuzo, pengine ni kwa sababu ya jina langu.” Alisema De Bruyne mara baada ya kukabidhiwa tuzo ya mchezaji bora wa mechi.

De Bruyne amesema hakustahili kushinda tuzo ya mchezaji bora kwenye pambano dhidi ya Canada

Katika pambano hilo Ubelgiji iliibuka na ushindi wa bao 1-0 bao lililofungwa na nyota wa zamani wa klabu ya Chelsea na Marseille Mitchy Batshuayi.

 

Katika hatua nyingine Kocha mkuu wa Timu ya Taifa ya Ubelgiji Roberto Martinez ambeibuka na kusema kuwa Canada ilikuwa timu bora kuliko Ubelgiji katika mchezo huo uliomalizika kwa Canada kukosa mkwaju wa penati baada mlinda mlango bora duniani kwa sasa Thibaut Courtois kupangua shuti la Alfonso Davies.

Leave A Reply