De Gea, Aumia, Hatihati Kuwavaa Liverpool

David de Gea.

MANCHESTER United wamekubwa na hofu kubwa kutokana na taarifa za kuumia kwa kipa wao mahiri David de Gea.

Kipa huyo aliumia juzi usiku wakati akiitumikia timu yake ya Taifa ya Hispania kwenye mchezo wa kufuzu michuano ya Euro dhidi ya Sweden.

 

Mashabiki wa timu hiyo wamekumbwa na hofu kubwa kutokana na majeraha hayo kwa kuwa wanaamini alikuwa na nafasi nzuri ya kuwasaidia kwenye mchezo wa wikiendi ijayo dhidi ya Liverpool.

 

Hii ni mechi muhimu zaidi kwa United msimu huu kutokana na timu hiyo kuanza vibaya na kumkosa De Gea ni pigo kubwa zaidi kwao.

Taarifa inasema kuwa kuna dalili chache kwa timu hiyo kumtumia kipa huyo wa Hispania ambaye amekuwa mahiri kwenye timu hiyo kwa miaka mingi.

 

Daktari wa timu ya Taifa ya Hispania amesema kuwa kipa huyo aliumia misuli na hivyo kulazimika kutolewa uwanjani kabla mchezo haujamalizika.

 

“Bado haijafahamika atakaa nje kwa muda gani, lakini jambo la kwanza ni kwamba alishindwa kuendelea na mchezo.

 

“Kuna hofu kuwa anaweza kukaa nje kwa muda mfupi ingawa ni lazima afanyiwe vipimo sahihi ndiyo tutasema muda kamili,” alisema daktari wa Hispania.

Toa comment