The House of Favourite Newspapers

‘Deal Done’: Mkhitaryan Asepa Arsenal, Sanchez Kuelekea Man U

Henrikh Mkhitaryan

TETESI zinaeleza staa wa Man U, Henrikh Mkhitaryan amekubali kujiunga na Klabu ya Arsenal ambapo sasa Alexis Sánchez anafanya mazungumzo ya kukamilisha uhamisho wake kuelekea kwa Mashetani Wekundu, Manchester United.

United, ambao walimnunua Mkhitaryan msimu wa 2016 kwa paundi £27 milioni, watalipa mkwanja kiasi cha paundi milioni £35 kwa Arsenal ili kunasa saini ya Sanchez.
Sanhez.

Mkhitaryan ameisadia United kunyakua Kombe la Europa na  EFL kwa misimu ambayo amekuwepo Old Trafford kabla ya Mourinho kumuondoa kwenye mipango yake msimu huu.

 

Mourinho alimuacha Mkhitaryan kwenye game ya jana usiku dhidi ya Stoke ambapo Man U waliibuka na ushindi wa bao 3-0. Mourinho alidai mchezaji huyo anafikiri zaidi uhamisho wake hivyo si wakati mwafaka kumchezesha.

Comments are closed.