DED WA ADAIWA KUUA MKULIMA KANISANI KWA RISASI – VIDEO

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Itigi, mkoani Singida, Pius Luhende na Askari wawili wanashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za kumuua mkulima Peter Chambalo kwa kumpiga risasi akiwa Kanisani.

 

Taarifa zisizo rasmi zinadai mkurugenzi huyo aliamuru Polisi kumpiga risasi mwananchi huyo ndani ya Kanisa la Waadventista Wasabato Itigi wakati ibada ikiendelea, chanzo kikidaiwa kuwa ni mgogoro wa ardhi.

 

Video iliyosambaa mitandaoni imeonyesha Jeshi la Polisi likiwa eneo la tukio na kulaani kitendo hicho na kuwataka wananchi wa Itigi wawe na amani huku likisema lazima waliofanya kitendo hicho washughulikiwe kwani hakun aliye juu ya sheria.

Loading...

Toa comment