The House of Favourite Newspapers

Dembele Aililia Miaka Mitano Aliyoipoteza Ndani ya Nou Camp

0
Ousmane Dembele akiwa anaugulia majeruhi

WINGA wa Klabu ya Barcelona na Timu ya Taifa ya Ufaransa Ousmane Dembele amefunguka juu ya maumivu aliyoyapitia katika miaka yake mitano ya awali akiwa na kikosi chake cha Barcelona.

 

Dembele ambaye kwa sasa yupo na kikosi cha Taifa cha Ufaransa kinachoshiriki michezo ya Uefa Nations amefunguka akidai kuwa miaka yake mitano ya awali akiwa na Barcelona ilipotea bure kwani alikuwa akiandamwa na majeruhi yaliyohusisha maumivu ya mara kwa mara ya misuli.

Ousmane Dembele akiwa na jezi ya Timu ya Taifa ya Ufaransa

“Kuanzia mwaka 2017-2021 nilipoteza muda wangu mwingi bure, nimepoteza miaka yangu mitano, ilinilazimu nifanye kazi zaidi ili niweze kucheza, niwe na afya na ili niweze kucheza kidogo kidogo.

 

“Nilikuwa nikisumbuliwa na maumivu ya misuli ya mara kwa mara. Mkufunzi wangu alinisisitiza zaidi kuwa kama sitafanya mazoezi ya kutosha maumivu yangeweza kujirudia, nikiwa na Koeman nilianza kupata unafuu lakini nikiwa na Xavi hali ndiyo imeimarika zaidi. Nilivyokuja Barca nilikuwa mdogo sana, na kimsingi najiachia ndiyo lakini siyo sana kama watu wanavyosema au wanavyoweza kufikiria.” alisema Dembele.

Dembele amepoteza miaka mitano kwa majeruhi akiwa na kikosi cha Barcelona

Tangu ajiunge na klabu hiyo ya Nou Camp kwa ada ya Euro Milioni 105 kutoka Klabu ya Borussia Dortmund, Dembele amekuwa akiandamwa na majeruhi ya mara kwa mara hadi hivi karibuni alipopata fursa ya kuepukana na majeraha na kuwa katika kiwango kikubwa akiisaidia klabu yake na sasa ameitwa katika kikosi cha timu ya Taif ya Ufaransa.

Leave A Reply