Na Mwandishi Wetu/ CHAMPIONI/GPL
MPENZI wa kipa wa Manchester United, David de Gea, Pushy Edurne Garcia, ameendelea kuonyesha kuwa kipa huyo yupo njiani kujiunga na Real Madrid baada ya kuonekana mjini Madrid akitafuta nyumba.
Mwanzoni mwa msimu uliopita, Madrid walionyesha nguvu kubwa sana ya kutaka kumsajili kipa huyo lakini walichelewa tarehe ya usajili huku timu zote zikiwa zimekubaliana kila kitu ingawa inaaminika Manchester United walibana.
De Gea alibaki na kuendelea kuichezea timu yake kwa uaminifu lakini Real Madrid inaelezwa kurudisha ndoano a kumnyatia.
Mwanadada huyo ameripotiwa kuwa alionekana mjini Madrid juzi akitafuta nyumba ambayo watakaa na De Gea kwa ajili ya kutengeneza familia.
Real wanalazimika kufanya mabadiliko ya kipa mwishoni mwa msimu huu kutokana na Keylor Navas kushindwa kuonyesha kiwango cha juu msimu huu, huku De Gea akipewa nafasi kubwa.
Comments are closed.