The House of Favourite Newspapers

Denti wa Kidato cha Kwanza Adungwa Mimba

0
Mjonba wa denti Denti wa kidato cha kwanza aliyebakwa.

STORI: Gladness Mallya | Risasi Jumamosi | Habari

DAR ES SALAAM: Denti wa kidato cha kwanza katika Shule ya Sekondari Kiyamwezi-Pugu jijini Dar, (jina linahifadhiwa) amejikuta kwenye wakati mgumu kufuatia ‘kudungwa’ mimba baada ya kurubuniwa kwa soda. Akizungumza na gazeti hili kwa huzuni, bibi wa mtoto huyo ambaye ndiye mlezi, Fatuma Seleman alisema amesikitishwa sana na kitendo cha mjukuu wake huyo kupewa ujauzito na mwanaume aliyefahamika kwa jina la Godfrey ambaye ni mtu na familia yake.

Denti wa kidato cha kwanza katika Shule ya Sekondari Kiyamwezi-Pugu jijini Dar aliyepigwa mimba.

“Nimeumia sana mjukuu wangu kuharibiwa maisha, mimi ni mjane sina uwezo, kipato changu ni kidogo, angalia na uzee huu huwa naenda Feri nachukua samaki nakuja kuuza huku Kipunguni, ndiyo napata fedha ya kula na wajukuu zangu kwani baba wa huyu mjukuu alishafariki dunia na mama yake ameolewa na mwanaume mwingine.

“Namuomba Rais Magufuli anisaidie niweze kupata haki ya mjukuu wangu kwani ameshaharibiwa maisha na mtuhumiwa alikamatwa akaachiwa kwa dhamana, vipimo vinaonesha kweli ana mimba kama ya miezi mitatu. “Wamekuwa wakija baadhi ya viongozi wa serikali ya mtaa wakitaka huyu mjukuu wangu akaitoe hiyo mimba ili kesi iishe tuyamalize lakini naogopa maana kutoa mimba ni hatari, naomba serikali inisaidie,” alilalamika bibi huyo.

Kwa upande wa denti huyo alidai kuwa, Godfrey anafanya biashara ya kioski hivyo kila alipokuwa akitoka shule alikwenda anakofanyia biashara, anampa soda baada ya hapo wanafanya mapenzi humohumo ndani ya kibanda cha biashara “Kila nikitoka shule alikuwa akiniita kwenye kibanda chake ananipa soda na hela elfu mbili au tatu za matumizi shuleni. “Kila siku nikitoka shule nikawa naenda kwa huyo baba tunazungumza na kufanya mapenzi ndiyo narudi nyumbani mpaka hivi karibuni nilipougua sana, nikagundulika nina mimba ambayo sasa ina miezi mitatu.

“Inaniuma sana kwa kweli maana ndoto zangu zote za kusoma zimeishia hapa kwani nilikuwa sijui kama nilichokuwa nafanya kitakuja kuniletea matatizo namna hii,” alisema denti huyo.

Mjumbe akitoa maelezo yake.

Mjumbe wa Shina la Kipunguni Magharibi, Shaban Maulid alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba limemuumiza kama mzazi kwani bibi wa mtoto huyo ana maisha duni pia ni mjane huku mjukuu wake huyo akiwa ameharibiwa ndoto zake.

Naye Mwenyekiti wa Mtaa wa Kipunguni, Prakseda Mkandara alithibitisha kupokea taarifa kutoka kwa walezi wa binti huyo na kwamba mtuhumiwa huyo alifikishwa kwenye Kituo cha Polisi cha Stakishari na kufunguliwa jalada la kesi lenye namba STK/RB/5079/17 KUBAKA. Akizungumzia tukio hilo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala, Salum Hamdan alisema kuwa, halijafikishwa mezani kwake.

Alipoulizwa kuhusu malalamiko ya wananchi juu ya mtuhumiwa kuendelea kudunda mtaani kwa dhamana, kamanda huyo alisema kisheria siyo tatizo hasa ikiwa upelelezi bado unaendelea.

Leave A Reply