Denti wa Kike ‘Aliyedeti ‘ Akutwa Amekufa

Mwanafunzi wa kike Megan Bannister enzi za uhai wake.

MWANAFUNZI wa kike Megan Bannister mwenye umri wa miaka 16 ambaye mwili wake ulikutwa katika gari dogo lililokuwa limeharibika katika ajali alikuwa amewadokeza marafiki zake kwamba angekuwa na kideti na mtu mmoja mzima.

Polisi wakiwa nyumbani alipokuwa anaishi Megan Bannister kabla ya kifo kumkuta.

Mwili wa Megan Bannister aliyekuwa amedhamiria kuwa mkunga baada ya kumaliza elimu yake, ulikutwa kiti cha nyuma cha gari dogo jeusi aina ya Vauxhall Astra baada ya kugonga bodaboda eneo la Enderby, Leicestershire, Uingereza.

Megan (kulia) aliyekuwa akiishi Leicester akiwa na mama yake Carol (katikati) na dada yake Kirsten.

Wapelezi walianza kushughulikia  suala la mauaji baada ya kuonekana kwamba majeraha ya msichana huyo ‘hayakuendana’ na tukio la ajali iliyotokea mnamo saa 5.45 Jumapili asubuhi.

Polisi akiwa nje akiendelea kuweka ulinzi.

Megan ambaye Jumanne wiki hii angefanya mtihani wake wa kwanza wa sekondari, alikuwa amewadokeza marafiki zake kwamba angekutana na mwanamume mmoja wenye miaka inayokaribia 30 kwenye klabu moja.

Wakati huohuoa likuwa amemdanganya mama yake Jumamosi kwamba anelala kwa rafiki yake.


Stori zinazo husiana na ulizosoma

Toa comment