The House of Favourite Newspapers

Dereva Bajaj afa ghafla!

0

IMG_1034Marehemu Deogratius Mlawa enzi za uhai wake.

Stori:  Suzan Kayogela, UWAZI

DAR ES SALAAM: Inauma sana! Deogratius Mlawa, mkazi wa Mlalakuwa, Mwenge Dar, amekutwa kwenye mfereji uliopo karibu kabisa na shamba la jirani yao akiwa amefariki dunia ghafla, baada ya kupatwa na kifafa na kuangukia jiwe lililosababisha kifo chake.

Tukio hilo la kuhuzunisha lilitokea saa kumi alfajiri ya Alhamisi ya wiki iliyopita, baada ya marehemu kurudishwa nyumbani jioni ya siku hiyo na rafiki yake akiwa ametoka kwenye kazi yake ya kuendesha Bajaj na kulalamika kwa mkewe kuwa kichwa kilikuwa kinamuuma.

IMG_1041 Mwili wa marehemu ukiagwa.

Akizungumza na gazeti hili, mke wa marehemu, Juliana Justine alisema baada ya kulalamika kuumwa kichwa mumewe alimeza dawa na kwenda kupumzika, lakini ilipofika saa kumi usiku alibaini  mumewe hakuwepo kitandani .

Alisema kuwa taarifa za mumewe kukumbwa na umauti alizipata asubuhi ya Alhamisi, baada ya jirani yao kuwafahamisha kuwa alikutwa amefariki dunia kwenye mfereji uliopo karibu na shamba jirani na nyumba yao akiwa amevaa bukta na kifua wazi.

IMG_8730Polisi wakiubeba mwili wa marehemu kutoka sehemu alikofia.

“Baada ya kupewa taarifa hiyo, tulikwenda na kushuhudia mume wangu akiwa ndani ya mfereji huo akiwa tayari amefariki dunia, mara nyingi alikuwa na tatizo la kuanguka.

“Siku hiyo aliporudi kazini alimeza dawa akaenda kupumzika chumbani, ilipofika saa kumi alfajiri nilishtuka usingizini na kukuta hayupo kitandani, niliingiwa na wasiwasi lakini nilisubiri hadi kupambazuke ambapo asubuhi tulipewa taarifa ya mume wangu kukutwa kwenye mfereji akiwa amefariki dunia,” alisema Juliana.

Naye mama mzazi wa marehemu, Mama Mlawa alipohojiwa na mwandishi wetu alisema:

IMG_8737…Mwili ukipakizwa kwenye gari.

“Nimeumizwa sana na kifo cha mwanangu, kilichosababishwa kuumwa sana kichwa akiwa shambani na kusababisha kuanguka na kupatwa na umauti, alikuwa na tatizo la kuanguka mara kwa mara.”

Marehemu Deogratius amezikwa katika Makaburi ya Sinza, Dar Januari 23, mwaka huu, ameacha mjane na watoto wawili.

Leave A Reply