The House of Favourite Newspapers

Dereva Mzembe wa Serikali Alivyoingia Kwenye 18 za Polisi – VIDEO

Jeshi la Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani kinafanya operesheni mbalimbali ili kuhakikisha kinapambana kuzuia ajali mbalimbali zinazotokea nchini ambazo hivi karibuni zimegeuka kuwa chanzo cha maauaji.

 

Operesheni hizo zinawelenga zaidi madereva wa viongozi wa serikali pamoja na wa magari ya serikali ambapo kwa kipindi kifupi yamepoteza maisha ya watumishi wengi.

 

Akizumgumzia operesheni hiyo RTO-Morogoro amedai kuwa katika kipindi cha mwisho wa mwaka kumbukumbu za usalama barabarani zinaonesha huwa kunakuwa na ajali nyingi kuliko katika vipindi vingine vya mwaka.

 

“Hii inatokana na kwamba wasafiri wengi hurejea majumbani mwao kipindi hichi lakini pia wanafunzi huwa wanaenda likizo.” aliongeza kuwa kwa kipindi cha mwisho cha mwaka huu wamejipanga ili kuthibiti tatizo hilo sugu.

Msikie Kamanda Musilimu Akifunguka

Comments are closed.