Dereva wa Mbunge wa CHADEMA Afariki Ajalini – Video

SINGIDA: Dereva wa Mbunge wa CHADEMA Lucy Magereri, Thomas Maro amefariki baada ya magari mawili kugongana likimwemo la Mbunge huyo eneo Issuna wilaya ya Ikungi mkoa wa Singida.

Katika gari la Mbunge alikuwepo dereva mwenye na alikuwa analitoa gari hilo Dodoma kulipeleka Shinyanga ndipo lilipogongana na Fuso lililokuwa linatoka Singida kwenda Dar.

Dereva wa Fuso amepata majeraha madogo madogo huku mwili wa marehemu ukihifadhiwa katika hospitali ya mkoa wa Singida.

Chanzo cha ajali hiyo ni dereva wa Fuso kuendesha gari upande ambao sio wake, na sasa amekamatwa yupo kituo cha Polisi kwa ajili ya mahojiano.

Loading...


Stori zinazo husiana na ulizosoma

Toa comment