The House of Favourite Newspapers

DHAMANA YA AMBER RUTTY MCHEZO UKO HIVI

 DAR ES SALAAM: Baada ya dhamana ya msanii Nascat Abubakar ‘Amber Rutty’ kuibua sintofahamu kwa baadhi ya watu, Amani linakudadavulia jinsi mrembo huyo pamoja na jamaa wake Said Mtopali, walivyofanikiwa kuwekewa dhamana hiyo kwenye kesi inayowakabili katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar.  

 

Awali, baada ya Amber Rutty kupata dhamana Novemba 27, mwaka huu na kuonekana ameambatana na Mchungaji Daudi Mashimo mahakamani hapo, watu wengi waliamini kwamba mchungaji huyo ndiye aliyemuwekea dhamana.

 

Mapema wiki hii, Amani lilizungumza na mama yake mkubwa Amber Rutty aitwaye Asha Seif ambaye alisema mbali na watu kuamini hivyo, alimshangaa Mchungaji Mashimo kuendelea kuwaamisha watu hivyo wakati si kweli.

 

“Mimi nashangaa, huyu mchungaji alikuja siku ile pale mahakamani akakuta mimi pamoja na wifi yangu tumeshakamilisha taratibu za dhamana, akaja huyo Mashimo, akaniambia anaomba anisaidie kumtoa nje Amber Rutty maana kuna fujo ya waandishi wa habari.

 

“Kwa kuwa mimi nilikuwa sijui sana mambo ya mahakamani, nikamkubalia kweli akafanya hivyo. Sasa baada ya kunisaidia, nikashangaa mara ooh sijui anampeleka kanisani, sijui mara atambadilisha dini, kwa kweli amenisikitisha sana,” alisema mama huyo. Alisema kwa jinsi alivyoona ni kama alikuwa anataka kujitangaza, hivyo alipomgundua akaanza kujitenga naye.

“Hivi ninavyokwambia huyo Amber Rutty na mwenzi wake wako hapa (Mtoni Mtongani jijini Dar), ninaishi nao mimi hayo mambo sijui ya kanisani sijui nini mimi siyajui. Mtu hawezi kuokoka au kubadili dini sababu ya matatizo, amuache kama atabadili kwa hiyari yake hapo sawa,” alisema mama huyo. Licha ya mama mkubwa huyo wa Amber Rutty kuonekana kumtolea povu mchungaji Mashimo, mchungaji huyo ameeleza ukweli wake kuwa yeye alimuwekea dhamana jamaa wake Amber Rutty, Said Mtopali.

 

“Mimi nilimuwekea dhamana Mtopali japo nilikuwa na lengo la kuwawekea wote wawili lakini bahati nzuri mama yake amemuwekea dhamana Amber Rutty basi mimi nikamuwekea Mtopali,” alisema Mchungaji Mashimo. Kuhusu suala la kujitangaza kumbadili dini Amber Rutty, Mchungaji Mashimo alisema ishu hiyo haina ukweli wowote kwani yeye alimkaribisha kwenye maombi na si kumbadili dini.

Mbali na Amber Rutty na Mtopali mshtakiwa wa tatu katika kesi hiyo ni James Charles maarufu ‘James Delicious’ tayari yupo nje kwa dhamana. Washtakiwa hao wanakabiliwa na makosa manne. Katika kosa la kwanza ni la kufanya mapenzi kinyume na maumbile ambalo linamkabili Amber Rutty, anadaiwa kutenda kosa hilo kati ya Oktoba 25, 2018 ambapo alimruhusu Mtopali kumuingilia kinyume na maumbile, kosa ambalo amelikana.

Katika shtaka la kufanya mapenzi kinyume na maumbile, linalomkabili Mtopali anadaiwa kati ama baada ya Oktoba 25, 2018 jijini Dar es Salaam alifanya mapenzi na Amber Rutty kinyume na maumbile. Kosa la tatu la kuchapisha video ama picha za ngono, linalomkabili James Charles ama James Delicious inadaiwa kati ya Oktoba 25, 2018, Charles alisambaza video za ngono kupitia makundi ya WhatsApp.

 

Kosa la nne ambalo ni kusababisha kusambaa picha za ngono linamkabili Amber Rutty na Mtopali wakidaiwa kati Oktoba 25, 2018 walisambaza picha za ngono kupitia makundi ya Whatsapp, jambo ambalo walilikana. Kesi hiyo itatajwa tena mahakamani hapo Desemba 10, mwaka huu.

Comments are closed.