Diamond Aanza Kupoteza Umaarufu

MWANAMUZIKI Diamond Platnumz wa Tanzania, anayefanya vyema kwenye ulimwengu wa muziki Bongo kwa maana muziki wa Bongo Fleva na nje ya mipaka ya Tanzania huenda ameanza kupoteza mvuto na ushawishi wake kwa mashabiki duniani kote baada ya kuzidiwa idadi ya mashabiki ‘followers’ kwenye mtandao wa kijamii wa Instagram huku aliyemzidi akiwa ni mpinzani wake wa karibu kwenye muziki barani afrika, mwanamuziki Davido kutoka nchini Nigeria.

927340_1508586932769536_1995268371_nMwanamuziki Davido wa Nigeria.

Mwanamuziki huyo wa Nigeria, Davido amefanikiwa kufikisha followers milioni 2.9 kwenye mtandao wake wa Instagram na kuwa muimbaji wa kwanza Afrika kuwa na followers wengi zaidi kwenye mtandao huo.

Mpaka wiki iliyopita nafasi hiyo ilikuwa ikishikiliwa na msanii wa Tanzania, Diamond Platnumz ambaye mpaka sasa ana followers milioni 2.7  kwenye mtandao huo lakini kwa sasa atashika nafasi ya pili.

14052427_1151071074963929_88878578_nMwanamuziki Diamond wa Tanzania.

Mpinzani wa karibu wa Davido, Wizkid ana followers milioni 2.5.

Waimbaji wengine wenye followers zaidi ya milioni moja ni:

Don Jazzy 2.2 milioni, Tiwa Savage 2.2 milioni, Vanessa Mdee 1.8 milioni, Alikiba 1.4 milioni na Yemi Alade 1.2 milioni.


Loading...

Toa comment