Diamond Funga Mwaka Concert…. Acha Kabisa! 

IMG_7177Mfalme wa muziki wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ akifanya yake usiku huu Dar Live.IMG_7181 IMG_7194 IMG_7212 IMG_7228 IMG_7242 Mashabiki wakifurahia.IMG_7262 IMG_7269 IMG_7270 IMG_7287Diamond akiendelea kukamua jukwaani.

WAANDISHI WETU

HISTORIA imeandikwa! Mkali wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ amevunja rekodi ya aina yake kwa kuangusha shoo baab’kubwa usiku wa kuamkia leo kwenye Ukumbi wa Dar Live, Mbagala Zakhem jijini Dar es Salaam.

Ratiba rasmi ya burudani ndani ya ukumbi huo ilianza jana asubuhi kwa michezo mbalimbali ya watoto, msanii wa nyimbo za uswahilini, Msaga Sumu, Wakali Dancers kisha Diamond akamaliza mchezo mzima.  Mapaparazi wetu waliokuwepo ukumbini humo; Chande Abdallah, Deogratius Mongella, Denis Mtima, Mayasa Mariwata, Andrew Carlos na

Musa Mateja waliripoti shoo hiyo moja kwa moja kwa bosi wao aliyekuwa makao makuu ya gazeti hili, Bamaga- Mwenge; wasikie mwenyewe: Saa 4:00 asubuhi

watoto dar live (7)MICHEZO YA WATOTO YATAWALA

Makao Makuu: Denis najua ume­ ka tangu asubuhi hapo ukumbini tuambie nini kimejiri hadi sasa.

Denis: Mkuu hapa tayari kumependeza, watoto wanazidi kumiminika wakiwa na wazazi wao. Wanacheza michezo mbalimbali kwenye mabembea, kuogelea na katika ndege maalum iliyopo ukumbini humu.

????????????????????????????????????

Makao Makuu: Piga kazi nitakurudia tena jioni.

Saa 10: 00 jioni

????????????????????????????????????

DIAMOND ‘AWASAPRAIZI’ WATOTO

Makao Makuu: Bila shaka Denis utakuwa na kitu, hebu tujuze.

Denis: Mkuu hapa watoto walikuwa bize na michezo yao lakini ghafla, Diamond akaibuka. Watoto wamepagawa. Wanamfuata anasindikizwa na mabaunsa.

Makao Makuu: Duh! Diamond kafata nini tena muda huu shoo si ni jioni?

Denis: Eee Mkuu lakini nasikia kaja kufanya ‘sound check’, sasa hapa ni nderemo na vi­ jo kwa watoto.

Saa 11:00 jioni

????????????????????????????????????

DOGO AIMBA WIMBO WA DIAMOND

Deogratius: Mkuu nakutafuta sana hupokei simu, nilikuwa nataka…

Makao Makuu: Unanitafuta kwani nimepotea, umenipata sasa leta maneno.

Deogratius: Mkuu ni hivi, kuna dogo mmoja kaomba kupanda jukwaani aimbe wimbo wa Diamond huu mpya wa Utanipenda. Sasa hapa Diamond mwenyewe kapagawa jinsi dogo alivyoonesha utundu wa kuimba na kucheza, huwezi amini Diamond kampa shilingi elfu hamsini papo kwa papo.

Makao Makuu: Madogo kama hao ndio wanatakiwa kuendelezwa, enhe nini kinaendelea tena baada ya tukio hilo?

????????????????????????????????????

Deogratius: Mkuu Diamond kava hizi ‘microphone’ za kisasa, anaanza kukagua jukwaa tayari kufanya maangamizi usiku wa leo.

Makao Makuu: Sa­ , huyo ni msanii wa Kimataifa, anajua wajibu wake.

Deogratius: Kila kitu kimekamalika, naona Diamond sasa anakwenda kubadili mavazi akisindikizwa na mabaunsa ili arudi kuja kufanya ‘vurugu’ zake.

Saa 4:30 usiku

wakali dancersWAKALI DANCERS WAFUNGUA SHOO

Makao Makuu: Enhe Andrew tuambie nini umekiona hapo mpaka sasa, umekuwa kimya muda mrefu.

Andrew: Mkuu sasa hivi ndiyo shoo inafunguliwa rasmi. Wakali Dancers, wakali wa ‘kusheki’ ndiyo wameanza baada ya undergrounds kumaliza kufanya yao jukwaani.

Saa 5:00 usiku

msagasumu akiimba wimbo wa shemeji unanitegaMSAGA SUMU AJIANDAA

Mayasa: Hapa namuona Msaga Sumu anajiandaa kupanda jukwaani Mkuu. Anaonekana amepania kweli kukinukisha.

Makao Makuu: Namjua huyo ana ngoma zake kama Na Huyu Mtoto, Shemeji Unanitega akiimba hizo itakuwa balaa.

Mayasa: Mkuu umetisha sana mi’nilijua unajua kuchapa hadithi tu kumbe hata nyimbo za Msaga Sumu unazijua! Mkuu ngoja nisogee kule nyuma getini naona kuna shangwe nahisi Diamond atakuwa anaingia ukumbini.

Saa 5:30 usiku

STARIC ALITAWALA JUKWAA

Makao Makuu; Enhe, huyo Msaga Sumu amepanda au nini kinaendelea sasa we Andrew?

Andrew: Mkuu sasa hivi ni zamu ya huyu chipukizi anayekuja kwa kasi ndani ya Bongo Fleva, Staric anafanya yake jukwaani. Anaimba wimbo wa mwisho.

Saa 5: 35 usiku

IMG_7989DIAMOND ATINGA UKUMBINI

Makao Makuu: Deogratius upo wapi mbona husomeki?

Deogratius: Mkuu nilikuwa huku getini, namuona Diamond anaingia na mabaunsa wake, full mbwembwe.

Saa 5:40 usiku

msagasumu akikamua ngoma ya huyu mtotoMSAGA SUMU AKINUKISHA

Makao Makuu: Mayasa upo?

Mayasa: Mkuu nipo, hapa namuona Msaga Sumu anamalizia shoo yake. Watu wanashangilia kweli zile ngoma zake za uswahilini. Wanaimba na kucheza naye pamoja. Anataka kushuka lakini mashabiki wanagoma, wanataka aendelee.

Makao Makuu: Hao nawajua, Msaga Sumu na Mbagala tena, hapo panachimbika sasa hivi.

Saa 5: 50 usiku

IMG_7260DIAMOND APANDA JUKWAANI

Mayasa: Mkuu hatimaye Diamond anakuja jukwaani. Ameanza na wimbo wa Nataka Kulewa, shangwe la hatari. Yani hapa ni shiiida watu wanagombania kuja kumshika mkono. Burudani ndiyo kwanza inaanza.

Makao Makuu: Natamani na mimi ningekuwepo ukumbini niinjoi kidogo!

Mayasa: Tayari wimbo wa kwanza umeisha, sasa anaimba wimbo wa Kizaizai, ni balaa. Watu wanapiga kelele kwelikweli. Wengine wanamfuatisha, yani hapa ni burudani kwa kweli.

Saa 6:20 usiku

ZARI345ZARI AWA GUMZO

Makao Makuu: Musa vipi upo humo ukumbini au umesinzia?

Musa: Nipo bosi wangu. Hapa sasa hivi Zari amekuwa gumzo wakati Diamond akiimba wimbo wa Mawazo, watu wanapiga kelele ‘Zarii..Zarii…Zariii.

Nahisi wanatamani angekuwepo ampe kampani mpenzi wake jukwaani.

Makao Makuu: Hahaha! Hao nao wana ‘mahaba’. Hawajamuulizia yule wa zamani? Nanilii… Sepetunga?

Musa: Hahah Mkuu uchokozi huo, mimi simo. Kifupi hapa ni bandika bandua, Diamond hana mpinzani Bongo aise. Ukumbi umejaa sijawahi kuona.

Shoo hii ya leo amevuja rekodi ya shoo ile ya mwaka jana. Huwezi amini, watu nasiki wameshindwa kuingia maana ndani kumefurika.

Makao Makuu: Huyo ndiyo Diamond, endeleeni kufuatilia kila kitu. Najua hapo ni burudani. Malizieni shoo, tukutane asubuhi o­ sini.

MKE WA MOSE IYOBO AIBUKA

Mayasa: Mkuu mbona unatuaga harakaharaka, huku namuona mke wa Mose Iyobo mzazi mwenzie na Aunt Ezekiel kaibuka nadhani kaja kumchunga mumewe asichepuke.

Makao Makuu: Hahaha, sasa atakuwa amechelewa sana, amchunge mumewe wakati alishachepuka na kuzaa nje ya ndoa, hicho si kichekesho, achana naye bwana we nenda kalale tukutane kesho kazini kama kawaida.

Mayasa: Sawa bosi usiku mwema.


Loading...

Toa comment