Diamond aibua mjadala kuoa wake 3!

DAR ES SALAAM: Kumewaka moto! Muda mfupi baada ya tetesi kusambaa mitandaoni kuwa staa grade one kunako Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ ana mpango wa kuoa wake watatu, ameibua mjadala matata, Gazeti la Ijumaa limedokezwa!

 

Hivi karibuni Diamond au Mondi anayetikisa kila kona na Wimbo wa Yope Remix akiwa ameshirikishwa na mwanamuziki Innocent Balume ‘Innoss’B’ mwenye asili ya Kongo DR, alikaririwa akisema licha ya kuwa na mpenzi ambaye ni mtangazaji wa redio mwenye uraia wa Kenya; Tanasha Donna, matumaini yake ni kuoa wanawake wawili au watatu mbele.

 

Staa huyo ambaye ni mmiliki wa Lebo ya Wasafi Classic Baby (WCB) aliwahi pia kuulizwa kuhusu kuonekana katika picha akiwa na warembo tofautitofauti kwenye hoteli mara kwa mara na kusema;

 

“Siyo kwamba napiga picha na warembo wa mjini hotelini mara kwa mara. Simba (mnyama) ukimuona ana ubora mkubwa, anaweza kuwa na wake wawili au watatu, lakini linapokuja suala la kumgusa tu umekwisha.”

Kauli hizo zimeibua mjadala mkubwa ndani na nje ya mitandao, ambapo kila mmoja amekuwa akisema lake.

 

“Diamond hapaswi kusema hivyo wakati tunajua ametulia na mpenzi wake Tanasha,” alikomenti mtandaoni shabiki mmoja aliyetambulika kwa jina la Shebby_shank.

 

“Ninavyojua mimi, Mondi hashindwi kufanya kweli japo ameongea kama masihara, lakini anamaanisha. Kama aliweza kuwa na Zari ambaye alizaa naye watoto wawili na kipindi hichohicho kumbe alikuwa akitoka na Mobeto na kuzaa naye mtoto, hilo halishindikani,” alikomenti shabiki Zuhura96.

 

“Kama namuona Mobeto vile akichekelea kwa jino la mwisho. Nani asiyependa kuwa mke wa pili kwa mfano?” Alikomenti shabiki mwingine, Juliana. ema20 na kuongeza kuwa dini yake ya Kiislam inamruhusu kuwa na hadi wake wanne.

 

Mondi, kabla ya kuwa na Tanasha, aliwahi kuwa katika uhusiano na mwanamama mjasiriamali wa Uganda, Zarinah Hassan ‘Zari The Bosslady’ na kubarikiwa kuwa na watoto wawili, Nillan na Tiffah.

 

Alishawahi pia kuwa katika uhusiano wa mwanamitindo Hamisa Mobeto na kuzaa naye mtoto mmoja, Dyllan huku wengine akiwapitia juu kwa juu bila kupata na watoto.

Stori: MWANDISHI WETU,Ijumaa


Loading...

Toa comment