The House of Favourite Newspapers

Diamond aingilia sakata la Nyosso, amchongea TFF

0

diamond1

Msanii wa muziki wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul, ‘Diamond’.

Wilbert Molandi,Dar es Salaam
WAKATI Juma Nyosso akisubiria hukumu kutoka kwenye Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), msanii wa muziki wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul, maarufu kwa jina la Diamond, amemvaa beki huyo wa Mbeya City, akidai huyo ni mmoja wa wachezaji wanaokwamisha soka la Bongo.

Kauli hiyo aliitoa hivi karibuni kupitia ukurasa wake wa Mtandao wa Kijamii wa Instagram, ikiwa siku chache tangu Nyosso amdhalilishe mshambuliaji na nahodha wa Azam FC, John Bocco.

Nyosso alifanya tukio hilo wikiendi iliyopita, wakati timu hizo zilipovaana kwenye Uwanja wa Azam Complex, Mbagala nje kidogo ya Dar es Salaam katika mechi ya Ligi Kuu Bara.

Kupitia mtandao huo, Diamond aliandika: “Wachezaji kama hawa ndiyo wanazidi kulitia dosari na kulididimiza soka la Bongo na kufanya tuzidi kuonekana mambumbumbu.

“Badala ya kupiga soka, unawaza kum…… mwenzio ili akipaniki apewe kadi nyekundu atolewe, kweli namna hii tutafika World Cup?” aliandika Diamond huku akiambatanisha na picha ikimuonyesha Nyosso akimdhalilisha Bocco.

Leave A Reply