Diamond Ali-miss Penza la Wema, Aanika Mazito

STAA wa Bongofleva kutoka WCB Wasafi, Diamond Platnumz amesema akitazama video ya wimbo wake mpya ‘Naanzaje’ analikumbuka penzi lake na Wema Sepetu.

Kupitia kwenye ukurasa wake wa mtandao wa Instagram, Diamond Platnumz ameandika ujumbe unaosomeka

“Nikiitazama hii video, hususan kipande hiki nakumbuka mbali sana… enzi za mahaba mazito na Madam, enzi ambazo tulikuwa tunajifungia chumbani wiki nzima, nakwepa ku-record na hata show ikitokea naitafutia sababu ya kutokuwepo…”

“Kiukweli wimbo huu wakati nautoa sikuuchukulia serious, niliutoa tu kama ‘bonus’ kwa kujua mashabiki zangu wameni-miss kunisikia nikiimba hivyo licha ya kupokelewa na kupendwa sana ulivyotoka…”

“For some reason kadri muda uendanvyo nimejikuta naupenda sana mbaya zaidi kila niusikiapo unanifanya nitamani tena kumpenda mtu na kuwa tena kwenye mahusiano japo ghafla akili timamu hunijiagna kunambia Simba jifocusie zako kwenye kazi mwaya.”


Toa comment